Friday, December 12, 2014

UVCCM inapinga vikali ukatili huu kwa watoto...


Nilikuwepo kumsaidia mtoto huyo...

UVCCM Mkoa wa Iringa, inapinga vikali ukatili huu kwa watoto. Hawa ndio taifa la kesho na UVCCM inaamini, bila watoto hakuna vijana wa leo  wala viongozi wajao..
Mtoto huyu wa mashine tatu,. manispaa ya Iringa alichomwa moto mikono yake na mama yake akituhumiwa kula mikate.
Njaa ilimuuma na jikoni aliona mikate, ungekuwa wewe ungefanyaje?
UVCCM kama mlezi wa chipukizi katika mkoa wa Iringa, inatoa wito kwa jamii kuacha ukatili kwa watoto.

Tunasikitika kupata takwimu za watoto waliofanyiwa ulawiti kwa mwaka huu inayofikia watoto 21, kwa miezi tisa.

Ukiona mtoto anafanyiwa ukatili, toa taarifa polisi ili mtoto huyo asaidiwe haraka iwezekanavyo.

 

MCHAGUE KIONGOZI BORA, CHAGUA CCM..

Vijana wenzangu wa mkoa wa Iringa, ninawatakia uchaguzi mwema wa Serikali za mitaa. Chagua CCM upate uwakilishi wa uhakika kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.

Ni CCM peke yake yenye mtandao wa uhakika wa uongozi kuanzia ngazi ya shina kwa maana ya nyumba kumi mpaka ngazi ya taifa.

Natoa wito kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM ili iwe rahisi kujiletea maendeleo yetu kwenye vitongoji, vijiji na mitaa.

Shime jitokeze ukapige kura, chagua CCM.

Tumaini Msowoya Kibiki

Mwenyekiti 

UVCCM

IRINGA

Thursday, December 11, 2014

IMETUPASA NA NI HAKI...

Hospitalini wapo wapiga kura wetu, imetupasa na ni haki kuwatembelea ili kujua afya zao na kuwaombea wapone haraka na kurejea nyumbani kwao...washiriki pamoja katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wednesday, December 10, 2014

UVCCM IRINGA KULA CHAKULA NA WATOTO YATIMA


MWENYEKITI wa UVCCM mkoa wa Iringa, Tumaini Msowoya Kibiki anatarajia kuandaa chakula cha mchana, kitakachowashirikisha watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa siku kuu za Christimass.

Akizungumza na mtandao huu, Msowoya amesema mara nyingi kundi hilo limekuwa likisahauliwa licha ya kuw,a lipo kwenye jamii.
Amefafanua kuwa, tangu alipoingia madarakani mwaka 2012, amekuwa akishirikiana na watoto wanapoishi kwenye mazingira magumu huku mkakati mkubwa ikiwa kuwasaidia vifaa vya shule ikiwemo ada.

MBUNGE WA CHALINZE ATOA WITO KWA MAKAMPUNI KUSAMBAZA HUDUMA KWA WATEJA WAKE

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (CCM) wanne toka kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Chalinze mjini Mkoani humo.

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani  Mh. Ridhiwani Kikwete,ametoa ushauri kwa Makampuni ya Mawasiliano  kufungua zaidi  vituo vya kutoa huduma kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom Tanzania lililopo  Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo.

Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya Ruvu,Miono,Gwata  wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imefungua duka jipya  katika  eneo la Chalinze.

Chalinze  ni moja ya kituo maarufu katika  mkoa wa Pwani ambacho wanapitia wasafiri wengi wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.

Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M Pesa na uuzaji wa bidhaa  za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Chalinze na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa  mballimbali na nje ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard   wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Anasema Richard

Vodacom ina mtandao wa maduka  85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa pwani
source
www.issamichuzi.blogspot.com

Tuesday, December 9, 2014

HUYU NDIYE JAKAYA MRISHO KIKWETE

Huyu ndiye Rais Kikwete wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Historia na haiba yake katika uongozi, ni elimu tosha kwa vijana wa kileo wanaotamani kuja kuwa viongozi siku za usoni.

Huwa najifunza mengi katika uongozi wa Rais wetu, Kikwete na nimeona niandike haya machache tuone alikotoka, jambo ambalo, pengine limemfanya awe kiongozi bora wa Tanzania katika nafasi yake ya Urais.

Rais Kikwete amezalia October 7, 1950 katika kijiji cha Msonga, Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani. Ni mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa.

Wazazi wake ni Halfani Mrisho Kikwete (Baba) na Asha Kayaka (Mama) ambao wametangulia mbele ya haki.

Alipata elimu ya msingi katika shule za Lugoba darasa la kwanza hadi la nane. Alisoma shule ya sekondari ya Kibaha kidato cha Kwanza mpaka cha nne mwaka 1966 hadi 1969.

Alimaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Tanga kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam mbako alitunukiwa Shahada yake ya kwanza ya masuala ya kiuchumi.

Alipata mafunzo ya uofoisa ya jeshi katika chuo cha uongozi wa jeshi Monduli, na kupata kamisheni ya kuwa Luteni na baadae kup[ata mafunzo ya ukombania katika chuo hichohicho.


HAIBA KATIKA UONGOZI

Kipaji cha uongozi cha Rais Kikwete kilianza kujitokeza katika maisha yake kuanzia shule ya kati, sekondari mpaka chuo kikuu kote alikuwa akiongoza wanafunzi wenzake.

Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kibaha, na baadae Naibu Kiranja mkuu wa shule ya Sekondari Tanga.

 Katika chuo kikuu cha Dar es salaam, Rais Kikwete alikuwa mwanaharakati wa siasa ambapo alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, wa chuo hicho upande wa mlimani huu ulikuwa mwaka 1973/74.

Katika nafasi yake hiyo alikuwa mstari wa mbele kutetea haki za wanafunzi na kuchochea vuguvugu la kuunga mkono harakati za ukombozi na kupinga sera za kibaguzi za makaburu, miongoni mwa wanafunzi na jumuia nzima ya chuo kikuu.

NDANI YA CHAMA

Ndani ya chama kipaji chake cha uongozi na moyo wa kujitolea kilionekana mapema tangu akiwa shuleni.

Alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU, katika shule ya sekondari ya Kibaha na Tanga. Alikuwa Mjumbe wa halmashauri kuu ya Umoja wa Vijana TANU Wilaya katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

 
Alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya Vijana wa CCM Taifa, na baadae alipohitimu masomo yake aliamua kujiunga na utumishi ndani ya CCM akiachana na utumishi wa Serikali au mashirika ya umma ambako kulikuwa na maslahi makubwa zaidi.

Alianza kazi akiwa katibu msaidizi wa Mkoa wa Singida, alipanda cheo na kuwa Katibu mtendaji wa mkoa. kote alikowahi kupangiwa kazi alitekeleza majukumu yake kwa ufanisi na uadilifu mkubwa.

Siku zote amekuwa kiongozi mshirikishaji na mwenye kujenga mahusian mazuri na viongozi wenzake na wale aliowaongoza.

Siku zote Rais Kikwete amekuwa mwaminifu kwa chama chake, amekuwa tayari kufanya kazi mahari popote na wakati wowote ambao amekuwa akitumwa.

Ni mwanamichezo na ni mtu mwenye mvuto na haiba kubwa huku akiwa na maono katika uongozi.

Alianza uongozi akiwa shuleni hadi sasa ni Rais wetu wa nchi, msikivu, mpenda watu, anayejituma na ambaye yupo tayari kuumia kwa ajili ya wengine.

 

Kikubwa kinachonivutia ni heshima kubwa aliyonayo kwa familia yake hasa mke, watoto na wengine wa nyumbani kwake.Ni nafasi nyingi sana amepitia katika uongozi, watanzania wanazitambua. 

Haiba hii, inamfanya kuwa kiongozi bora nje akianzia katika familia yake. Ni muwazi na kiukweli, amemrithisha mwanaye Ridhiwani Jakaya Kikwete ambaye nyota yake imeanza kuwaka, na inawaka vyema ikiwavutia vijana wengi.

Mungu Mbariki Rais Wetu Jakaya Kikwete, Ibariki familia yake na ulibariki Taifa hili.

Amen.